Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Kuhusu TCRA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi iliyoasisiwa kwa mujibu wa sheria yenye wajibu wa kudhibiti sekta ya Mawasiliano ya Kielektroni na Posta Tanzania.

DIRA YETU
Jamii iliyowezeshwa na huduma za mawasiliano.

DHAMIRA YETU
Kusimamia huduma za mawasiliano kwa ustawi wa Jamii ya Watanzania.

WAJIBU WETU
Wajibu wa Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni kudhibiti sekta ya mawasiliano na kielektroni na posta kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Namba 12 ya mwaka 2003