KANUNI NA MUONGOZO

Watani wa Jadi ni Channel ambayo inazingatia weledi na maadili yanayoongoza tasnia ya habari. Tumejikita katika Nyanja ya Michezo hususani klabu mbili za YANGA na SIMBA ambazo zenyewe zina ushindani mkubwa na pia ni watani wa jadi Tunazingatia misingi ya uhariri katika habari kwa kufuata yafuatayo:

1. Kuripoti habari za ukweli zenye kufuata misingi ya habari zenye uwiano na kutoa fursa sawa kwa pande zote .
2. Kusaidia kurekebisha taarifa zilizopotoshwa ili kuwapa ukweli wafuatiliaji wetu.
3. Kujiepusha na udini, ukabila au mambo yoyote yanayoweza kusababisha uchochezi.

Muongozo kwa Wafuatiliaji Wetu (GUIDELINES FOR OUR SUBSCRIBERS)

1. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.
2. Watani wa Jadi ina uhuru wa kufuta maoni yasiyo na maadili au yenye matusi.
3. Watani wa Jadi ina uhuru wa kumzuia mfuatiliaji aliyekiuka masharti asiweze kuona habari zetu au kuweza kuweka maoni.

ONYO: Ni Kosa kujimilikisha Maudhui/Contents za Watani wa Jadi, COPYRIGHT STRIKE ITAKUHUSU.


Watani wa Jadi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, amewataka mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kujtokeza kwa wingi kesho Jumapili kwenye Uwanja wa KMC Complex!

Mechi dhidi ya KMC si ya kawaida, hii ni mechi ya heshima, mechi ya kuwaaga mashujaa wetu kabla hawajapaa anga kwenda kuwakilisha taifa kwenye ardhi ya Morocco, katika fainali ya CAF Confederation Cup dhidi ya RS Berkane!

7 months ago | [YT] | 3

Watani wa Jadi

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana na kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake, ikiwemo lile lililomhusu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe.

Katika shauri hilo, Kamwe alituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma, na baada ya uchambuzi wa kina wa ushahidi uliowasilishwa, Kamati imemtia hatiani na kumtoza faini ya Shilingi Milioni 5. Aidha, amekabidhiwa onyo kali la kutofanya kosa lolote la kimaadili kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe ya uamuzi huo.

8 months ago | [YT] | 2

Watani wa Jadi

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwachia huru Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, baada ya kutokumkuta na hatia katika shauri lililofunguliwa dhidi yake na Klabu ya Yanga.


Ahmed Ally alishtakiwa kwa tuhuma za kuchochea umma kinyume na Kanuni ya 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF, Toleo la mwaka 2021. Hata hivyo, baada ya Kamati hiyo kukutana na kupitia ushahidi uliowasilishwa na pande zote, ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kosa hilo.


"Baada ya kupitia maelezo ya pande zote husika pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, Kamati ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumuingiza hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo, na hivyo imemuachia huru," ilieleza taarifa rasmi ya Kamati ya Maadili ya TFF.


Kwa msingi huo, Ahmed Ally ameondolewa rasmi katika mashitaka hayo na ataendelea na majukumu yake kama kawaida ndani ya klabu ya Simba SC.

8 months ago | [YT] | 5

Watani wa Jadi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya mechi za nusu fainali ya Kombe la CRDB, ambapo timu ya Simba itachuana na Singida Black Stars kati ya Mei 16 hadi 18 katika Uwanja wa Tanzania Kwaraa, mkoani Manyara.

Kabla ya mtanange huo, kutachezwa mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya Yanga na JKT Tanzania, ambayo imepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, mkoani Tanga.

8 months ago | [YT] | 2

Watani wa Jadi

Mapema Jumatano, Aprili 16, kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kutua visiwani Zanzibar kuanza rasmi kambi ya maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.

Wekundu wa Msimbazi watakuwa na takribani siku nne za kujifua kikamilifu kabla ya kushuka dimbani Jumapili, Aprili 20, kwenye Uwanja mpya wa New Amaan Complex, ukiwa ni mchezo wa kihistoria kwa klabu hiyo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ali, amesema kikosi kimepania kuhakikisha kinafikia fainali ya michuano hiyo na hatimaye kutwaa taji, jambo ambalo litaongeza nafasi yao kwenye viwango vya CAF ambapo kwa sasa wameshika nafasi ya nne barani Afrika.

8 months ago | [YT] | 4

Watani wa Jadi

Klabu ya Yanga SC imeonyesha ubabe wa hali ya juu baada ya kuichakaza Stand United kwa mabao 8-1 na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Waungaji wa Magoli hayo ni Stephane Aziz Ki (4), Nickson Kibabage, Clatous Chama (2) na Kennedy Musonda.

8 months ago | [YT] | 0

Watani wa Jadi

Rais wa Heshima wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji, ameandika ujumbe wa pongezi kupitia mtandao wake wa kijamii, akisema "Alhamdulilah, Tumevuka" ikiwa ni ishara ya furaha na mafanikio kwa timu hiyo.

9 months ago | [YT] | 8

Watani wa Jadi

MTAKE AU MSITAKE MKUDE ATAAGWA SIMBA DAY | MAMBO YAMESHAKUWA MAZITO

2 years ago | [YT] | 0

Watani wa Jadi

Hiki ndicho Mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele amekiandika kupitia ukurasa wake wa instagram.

"Tukutane kwa Mkapa"

Kilele cha Wiki ya Mwananchi ni kesho Jumamosi kuanzia saa 5:00 asubuhi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

#watani #wataniwajadi

2 years ago | [YT] | 0

Watani wa Jadi

Jezi namba sita imekuwa maarufu sana, ule wakati wa kumfahamu muhusika wake umefika!, Ni suala la muda tu Yanga itamtangaza mchezaji aliye nyuma ya jezi hiyo ambaye atakuwa 'surprise' kubwa kwa mashabiki

ENDELEA KUWA NASI HAPA HAPA #wataniwajadi LEO

2 years ago | [YT] | 1