Mchuchuma TV ni channel ya mtandaoni inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kupitia *video na sauti*.
Channel hii inalenga kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha jamii kwa kuangazia masuala mbalimbali muhimu yakiwemo:
* Kilimo na ufugaji(Lengo kuu)
* Maendeleo ya jamii
* Utunzaji wa mazingira
👉 Karibu sana kujiunga na familia ya *Mchuchuma TV Online*.
Tafadhali *usisahau kubonyeza Subscribe*, kisha *alama ya kengele* ili kupata taarifa kila tunapotoa video mpya.
Pia *Like, Comment na Share* video zetu ili kutusaidia kufikisha elimu kwa watu wengi zaidi.
📞 *Wasiliana nasi:*0628 710 325
Asante kwa kutuunga mkono🙏
www.instagram.com/mchuchuma_tv?igsh=dndsYTMwNmY3NH…
Mchuchuma tv
Je wajuwa zao lenye pesa ndefu?
Hili ni zao lenye pesa nyingi sana Tanzania,Debe moja liliuzwa zaidi ya shilingi laki moja na ishirini 12,0000 kwa Msimu wa mwaka Jana 2025-2026 lakini halizungumziwi kwa kina kaa- tayari wiki hii nakuleletea makala malum(dude), karibu nipe unachotaka kukijua kuhusu kahawa hutojutia kutazama makala hii kupitia You tube ya #mchuchumatv Mimi ni #maikomwlimama #mbozifinest
3 weeks ago | [YT] | 7
View 0 replies
Mchuchuma tv
Mtazamaji wa #mchuchuma tv online unataka nikuletee kitu Gani Kutoka kwenye Kilimo Cha parachichi, tufuatilie kupita YouTube
link-youtube.com/@mchuchumatv-mwamlima-dulle?si=UumiTMC… utapata habari zote zianzohusu Kilimo Cha parachichi
2 months ago | [YT] | 15
View 7 replies
Mchuchuma tv
Dhahabu ya kijani taja Mkoa unaozalisha parachichi Tanzania
1 year ago (edited) | [YT] | 2
View 1 reply
Mchuchuma tv
SERIKALI YA SAMIA YATUMIA BILIONI 187 KUSAMBAZA UMEME MTWARA, VIJIJI VYOTE VYAFIKIWA
Ni furaha na nderemo kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufanikiwa kufikisha umeme katika Vijiji vyote 785 vilivyopo katika Mkoa huo.
Serikali imehitimisha kazi Oktoba 28,2024 ya kuwasha umeme katika kijiji cha Makome A ambacho ndio kijiji pekee kilichokuwa hakina umeme.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameipongeza REA kwa kufanikisha ndoto hiyo.
“Tunapenda kumpongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha kwa vipindi tofauti kuhakikisha historia hii inaandikwa. Sasa tuna deni kubwa kama wananchi wa Mtwara kuhakikisha tunatumia umeme huu kujiletea maendeleo yaliyokusudiwa,” amesema.
Kanali Sawala pia amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya umeme kwa kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia imetumia gharama kubwa sana kufanikisha miundombinu hiyo kufika katika makazi yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vya Mtwara kutumia kipindi hiki cha mauzo ya korosho kuhakikisha nyumba zao zinafanyiwa maandalizi ya kuingizwa umeme na kuunganisha na umeme huo wa REA ili malengo ya serikali yafikiwe.
“Gharama ya kuunganisha umeme huo ni 27,000 tu, bei nafuu ambayo ni kodi wakati gharama zingine zote serikali imezibeba ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.
"Tutumie uwepo wa umeme huu kujieletea maendeleo ya kiuchumi,” amesisitiza Balozi Kingu.
Awali akitoa taarifa kuhusu miradi ya REA katika mkoa huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu amesema kuwa Wakala kupitia miradi mbalimbali iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 187 imewezesha vijiji vyote 785 kupata umeme.
Mhandisi Olotu ameongeza pia baada ya kukamilika kupeleka umeme katika vijiji sasa wakala umeanza safari ya kupeleka umeme katika Vitongoji na kuwahamasisha wananchi kuendelea kutumia umeme huo kujiletea maendeleo yaliyokusudiwa.
“Mwaka 2021 vijiji 384 tuu ndio vilikuwa na umeme. Ndani ya miaka mitatu tumefanikiwa kupeleka umeme katika vijiji 401 na hivi sasa vijiji vyote 785 vina umeme.
"Kwenye upande wa vijiji hatuna deni. Lakini sisi kama REA hatujaishia hapo na sasa safari ya kupeleka umeme katika vitongoji imeanza.
Mkoa wa Mtwara una vitongoji 3,427 na mpaka sasa vitongoji 2,200 ndio vina umeme.
"Tayari tunawakandarasi wanaendelea kupeleka umeme katika vitongoji, tuwaombe wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao na Wakala kwa ujumla,” amesisitiza Mhandisi Olotu.
#KAZIINAONGEA
1 year ago | [YT] | 4
View 0 replies