Is an online television registered with the Tanzania Communications Regulatory Authority -TCRA for reporting all news, information, social events, politics, economics, sports and development around the world, our registration number is TCRA/OCS-OT/074/2018.

In addition Gilly Bonny Tv reserves the right to delete any comments that violate the laws, policies and guidelines of the State or YouTube.

Ni runinga ya mtandaoni iliyosajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA kwa ajili ya kuripoti habari zote, taarifa, matukio ya kijamii, siasa, uchumi, michezo na maendeleo duniani kote, namba yetu ya usajili ni TCRA/OCS-OT/074/2018.

Aidha Gilly Bonny Tv ina haki ya kufuta maoni ya mtu yoyote yanayokiuka sheria, sera na miongozo ya Nchi na youtube.

Contacts
Email: gillybonny1991@gmail.com
phone: +255655832712
WhatsApp: +255655832712




Gilly Bonny Tv

Jumuiya ya Watanzania waishio nchini China (DITAG) ditag_china imekabidhi rasmi Rasimu ya Mapendekezo na Ushauri kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rasimu hiyo ilipokelewa kwa niaba ya Rais na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabiti Kombo, alipokuwa ziarani nchini China hivi karibuni kuhudhuria mikutano ya kimataifa.

Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Guangzhou katika mkutano uliohusisha Ubalozi wa Tanzania nchini China, uongozi wa DITAG pamoja na Waziri Kombo.

Jumuiya hiyo iliwasilisha rasimu hiyo kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi yao kwa Rais Samia, waliyoitoa wakati wa ziara yake nchini China mnamo tarehe 6 Septemba 2024, ambapo alikutana na Watanzania waishio China akiwa kwenye mkutano wa FOCAC uliofanyika jijini Beijing.

Rasimu hiyo, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa DITAG, Ndg. Hashim Shelali, pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Ndg. Alawi Abdallah, @decent_4.0 kwa niaba ya wanajumuiya wote, inajumuisha pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa juhudi zake katika kukuza mahusiano ya kimataifa, kuvutia uwekezaji na kuimarisha sekta mbalimbali za kiuchumi, elimu na utalii.

Vilevile, rasimu hiyo imebeba mapendekezo na ushauri kwa Serikali kupitia wizara mbalimbali kama vile Wizara ya Mambo ya Nje, Maliasili na Utalii, Biashara na Viwanda, Fedha, pamoja na Kilimo.

Mapendekezo hayo yanalenga kuongeza tija katika maeneo ya biashara ya bidhaa za Tanzania nchini China, kuhamasisha utalii, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuendeleza elimu ya juu na ushirikiano wa kiteknolojia, pamoja na kuchochea biashara ya madini na bidhaa za kilimo.

Makabidhiano haya yalifanyika sambamba na ziara ya Waziri Kombo nchini China ambapo pia alihudhuria Mkutano wa Mawaziri wa FOCAC kuhusu utekelezaji wa maazimio ya ushirikiano kati ya China na Afrika pamoja na Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Biashara kati ya China na Afrika yaliyofanyika jijini Changsha.

DITAG inaamini kuwa rasimu hiyo itatoa mchango chanya katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China na kuchochea maendeleo endelevu kwa manufaa ya Watanzania wote.

5 months ago | [YT] | 10

Gilly Bonny Tv

https://youtu.
be/L-zr4lY7qN0?si=R-YeTLU3Of4ni2_R

7 months ago | [YT] | 3