Focus News Tanzania Tv 1, ni channel yako ya TV ya kiganjani ambapo utapata habari mbalimbali ikiwemo habari za kijamii, Siasa, Michezo na Burudani bila kusahau mahojiano katika mada mbalimbali.
Tupo Dodoma Makao Makuu ya Tanzania maeneo ya Ipagala jirani na kanisa la kwa Evance. Jiunge nasi kwa kubonyeza mandishi mekundu yaliyoandikwa Subscribe na kisha bonyeza alama ya kengere na hapo utakuwa umeungana nasi mubashara.
Akhsante kwa kuendelea kuichagua Focus News Tanzania kuwa channel yako pendwa ya TV ya kiganjani.
Focus News Tanzania Tv 1,
Mobile:.+255755834996
Whatsapp:β¦.+255755834996
E-mail:...focusnewsroomtanzania@gmail.com
Focus News Tanzania Tv 1
MSIGWA AWAANGUKIA WAZEE TARIME, AFICHUA MAMBO MAZITO AMTAJA LISSU.
πππππππ
https://youtu.be/OL8twotekJo
3 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
RUBANI SMIT MACHHAR, ALIYEINUSURU NDEGE YA DUBAI KUELEKEA ISRAEL
Rubani wa ndege ya Flydubai, Kapteni Smit Machhar, ameibua gumzo duniani kutokana na 'ujasiri' aliouonyesha wakati wa safari ya ndege kati ya Dubai na Israel.
Machhar, raia wa India, amepongezwa na viongozi mbalimbali duniani, akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.
Kwa mujibu wa taarifa, Kapteni Machhar alishambuliwa kwa kisu ndani ya ndege ya Flydubai nambari FZ1073.
Inadaiwa kuwa alifanikiwa kufungua mlango wa chumba cha marubani kabla ya kupoteza fahamu kutokana na majeraha aliyoyapata katika shambulio hilo.
Inaripotiwa kuwa ajali ya ndege iliepukika kutokana na hatua zao za tahadhari katika mazingira magumu sana.
Yaniv Hayun, abiria raia wa Israel aliyekuwa kwenye safari hiyo, alitoa taarifa hizo wakati akizungumza na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion siku ya Jumatano Septemba 30
ππππππππ
https://youtu.be/pAaMbX1urmo
3 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
#LIVE: HECHE ANAUNGURUMA SIKU YA WAZEE DUNIANI.
ππππππππ
https://youtu.be/HRN_XjkSBFk
3 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IKULU YA MAREKANI YAWARUHUSU TENA CNN, MS NOW NA POLITICO
Ikulu ya Marekani imeruhusu tena waandishi wa CNN, MS NOW na Politico kuingia katika eneo la Ikulu baada ya jaji kuamuru warejeshewe ruhusa hiyo.
Jaji wa Marekani, Tim Kelly, alisema uamuzi wa Rais Donald Trump kuwazuia waandishi wa vyombo hivyo huenda ulikuwa kinyume na Katiba ya Marekani.
Jaji huyo aliamuru zuio hilo lisitishwe kwa siku 14 wakati kesi hiyo ikiendelea.
Hata baada ya amri hiyo kutolewa, waandishi hao walizuiwa kuingia Ikulu kwa muda siku ya Alhamisi. Hali hiyo ilisababisha vyombo hivyo vitatu kuomba jaji asikilize suala hilo haraka.
Baadaye Ikulu ilianza kurejesha vitambulisho na ruhusa za waandishi hao.
ππππππππ
https://youtu.be/UVNF-pLDIiI
1 week ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
RAIS WA CHINA XI JIPING AMUONYA TRUMP AWE MAKINI KUHUSU TAIWAN
Rais wa China, Xi Jinping, amemtaka Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa makini katika kushughulikia suala la Taiwan.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua, Xi amesema China inatarajia Marekani kusimamia msimamo unaopinga Taiwan kujitenga na China.
Xi ameitaka Washington βkushughulikia kwa umakini suala la Taiwanβ, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Marekani.
πππππππ
https://youtu.be/8tkQ_0412dQ
1 week ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IRAN: ENZI YA NDEGE ZA KIVITA ZA MAREKANI KUFANYA OPERESHENI BILA KUTISHIWA IMEKWISHA
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema enzi ambayo ndege za kivita za Marekani aina ya F-35 na F-15 zingeweza kufanya operesheni bila kukabiliwa na tishio la kuwindwa imekwisha, akisema taarifa za ndege hizo kuharibiwa na sasa zimekuwa hali mpya ya kila siku kwa Washington.
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye akaunti yake ya X, Qalibaf alijibu kauli za hivi karibuni za mkuu wa jeshi la Marekani, akisema kile ambacho hapo awali kilikuwa βjinamizi kubwaβ sasa kimekuwa uhalisia.
βEnzi ambayo F-35 na F-15 zenu zinawindwa na kulazimika kuripotiwa kuwa zimeharibika tayari imeanza,β Qalibaf aliandika.
βKile ambacho hapo awali kilikuwa jinamizi kubwa sasa ni hali ya kila siku. Ishini nayo,β aliwakumbusha maafisa wa Marekani.
Ujumbe wake ulikuja baada ya Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi ya Marekani, Jenerali Dan Caine, kusema katika hotuba kuu kwenye Mkutano wa Anga, Anga za Juu na Mtandao (Air, Space and Cyber Conference) kwamba vikosi vya jeshi la Marekani sasa lazima viwe tayari βkuwindwaβ na mifumo inayojitegemea, kukabiliwa na usumbufu wa mawasiliano ya kielektroniki na kufuatiliwa kwa wakati halisi.
ππππππππ
https://youtu.be/DMvE5s-28R8
2 weeks ago | [YT] | 0

MANDAMANO IRAN, MAELFU WAMIMINIKA BARABARANI KUIUNGA MKONO SERIKALI.
Mamia ya maelfu ya Wairani wameandamana mjini Tehran kuunga mkono serikali na kuahidi kuilinda nchi yao, huku Tehran ikidai kushambulia meli ya mafuta katika Mlango Bahari wa Hormuz.
Mamia ya maelfu ya Wairani walijitokeza Ijumaa katika maandamano yaliyoandaliwa na serikali mjini Tehran. Haya ni miongoni mwa maandamano makubwa zaidi tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Februari.
Washiriki walitembea katikati ya jiji wakiwa wamevalia sare za kijeshi na kubeba bendera za taifa. Serikali ya Iran inasema kampeni hiyo, inalenga kuwatayarisha raia kushiriki katika ulinzi wa nchi wakati vita na shinikizo la kiuchumi vinaendelea.
Mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi mjini Tehran, Jenerali Hassan Hassanzadeh, amesema zaidi ya watu laki sita wamejisajili kushiriki mafunzo ya kijeshi, huku zaidi ya milioni moja wakitarajiwa kushiriki baadaye. Takwimu hizo hazijaweza kuthibitishwa kwa njia huru.
Katika maandamano hayo, viongozi wa juu wa kisiasa na kijeshi, akiwemo Rais Masoud Pezeshkian, walihudhuria. Hossein Taeb ni mkuu wa kikosi cha kijeshi kiitwacho Basij
ππππππ
https://youtu.be/HOLMfEpWV2U
2 weeks ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
#LIVE: AFISA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA VIPIMO TANZANIA ANAZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI MUDA HUU.
ππππππ
https://youtu.be/b0CmZM8-1Vg

Load more