Bantuadventurestv

Number one African channel for tourism and travel news.we are dedicated to bring to you documentaries of places that you never been before.history and many more.


Bantuadventurestv

Moja ya urithi wa dunia wa UNESCO ni mji wa zamani wa Songo Mnara,mji huu yasemekani ulivumbuliwa mwishoni mwa karne ya 14 katika eneo la Kilwa kisiwani katika mkoa wa Lindi Tanzania.

Mji huu ulikuwa kitovu kikubwa cha biashara katika bahari ya Hindi wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali duniani kama China na India walifika eneo hilo kubadilishana bidhaa tofauti tofauti.


#bantuhistoria #bantunews #bantuadventurestv #bantuupdate #kilwakisiwani #songomnara

1 year ago | [YT] | 1

Bantuadventurestv

HADZABE-Nikabila ambalo limetawaliwa na uwindaji kwa sehemu kubwa.

Wanapatikana maeneo yanayozunguka bonde la ziwa Eyasi na jirani ya uwanda wa mbuga ya Serengeti nchini Tanzania.

Moja ya kivutio katika kabila hili ni kwamba uishi katika kambi ambazo zinakuwa na idadi ya watu wasio pungua 20-30 na maamuzi kuhusu shughuli zao za kila siku ufanywa kwa makubaliano.

Ulazimika kuhama kuweka kambi eneo lingine pindi mmoja wao anapofariki au anapougua sana.

Chakula chao pendwa ni nyama ya ngedere na upenda kuisifia kuwa ni "nyama tamu"

#bantuhistoria #bantunews #bantuadventurestv #bantuupdate #hadzabe

1 year ago | [YT] | 2

Bantuadventurestv

Usikose kujiunga nasi live leo saa 12:00 jioni katika maadhimisho ya miaka 10 ya Shilo Praise katika Youtube channel yetu ya BANTU ADVENTURES TV
#bantuadventures #bantuupdate

2 years ago | [YT] | 5

Bantuadventurestv

Tamasha la Utamaduni wa kabila la #Wamatengo Mkoani #Ruvuma litafanyika kila mwaka ili kutangaza utamaduni wa kabila hili la Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Tanzania.


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo wakati akifungua tamasha hilo katika kijiji cha Makumbusho Mtama Wilayani #Mbinga.


Matamasha haya yanatangaza Utalii, Utamaduni, Mila na Desturi zetu watanzania, tamasha hili lifanyike kila mwaka ili kukumbushana maisha yetu ya asili,pia nitoe rai kwa makabila mengine kuwa na Matamasha kama haya katika maeneo yao.


Tamasha hilo lilishereheshwa na burudani mbalimbali na kupambwa na maonesho ya tamaduni zenye asili ya kabila hilo.


Kwa taarifa zaidi tafadhali usikose kutembelea YOUTUBE CHANNEL yetu kwa jina BANTUADVENTURES TV.


#bantuupdate #bantuadventurestv #travel #tourism #ruvuma

2 years ago | [YT] | 1

Bantuadventurestv

Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa masuala ya Wanyamapori, na Misitu.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Angellah Kairuki baada ya kufungua mkutano wa 24 wa Kamisheni ya Afrika ya Misitu na Wanyamapori (AFWC24) amesema hii ni heshima kubwa kwani kati ya nchi 53 ambazo ndio wanachama wa kamisheni hiyo, nchi 40 zimetuma wawakilishi wake .


Hata hivyo hadi sasa tuna washiriki takriban 300 , lakini wapo pia wengine ambao watashiriki kupitia njia ya mtandao, Tunaamini watanufaika kwa Watanzania Wataalam kutoka serikalini wanao simamia masula haya, watakuwa pia na majadiliano mahususi kuhusiana na biashara nzima ya hewa ukaa.


Mh.Kairuki amesema Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Wanyamapori Tanzania (2007), inayotaka Uhifadhi wa Wanyamapori na makazi yao pamoja na matumizi endelevu ya Rasilimali za Wanyamapori Nchini.


Utekelezaji wa sera hiyo umewezesha mtandao wa maeneo ya hifadhi Tanzania kukua na kufikia Hifadhi za Taifa 21, Eneo 1 la Hifadhi, Mapori ya Akiba 29, Mapori Tengefu 25, Maeneo 22 ya Hifadhi za Wanyamapori.


Pia Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Kairuki amesema Tanzania ilishinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa Kongamano la 50 la Apimondia litakalofanyika Jijini Arusha mwaka 2027,hivyo anawakaribisha wadau kuhudhuria mkutano huo.


Wageni hao mara baada ya mkutano huu watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo jijini Arusha na vile vilivyopo nje ya jiji la Arusha.


Kwa taarifa zaidi tafadhali usikose kujiunga na YOUTUBE CHANNEL yetu kwa jina BANTUADVENTURES TV na mitandao yetu ya kijamii INSTAGRAM na TWITTER.


#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews #tourism #travel

2 years ago | [YT] | 3

Bantuadventurestv

Wanyama hawa wana jamii ya paka, wanyama hawa wanaochanganya sana hasa ukiwatizama kwa haraka ni kama wanafanana sana, lakini wanatofautiana sana.


Vitu vinavyowafanya wafanane kwenye maeneo mengi ni wote ni wanyama pori jamii ya paka ,wote wanazaa na kunyonyesha
kitaalamu wanaitwa (mammals) na wote hawa ni wanyama wanaokula nyama kitaalama wanaitwa (carnivores)


Rangi ya ngozi zao zina fanana kwa muonekano wake zina rangi ya manjano inayofanania na rangi ya dhahabu yenye madoa ambayo yameungana nakutengeneza mduara na madoa meusi,pia Duma uso wake una alama ya machozi huku #Chui akiwa hana alama hizo


Chui wana miili mikubwa na miguu mifupi yenye ujazo na wana vichwa vikubwa ,huku Duma akiwa na utofauti
mkubwa hawa wana miili myembamba (Slender bodies) miguu mirefu myembamba na vichwa vidogo.

Katika hili #Duma yuko tofauti sana na wenzake yeye ni mchangamfu zaidi wakati wa mchana kwa sababu yeye ana uwezo wakuona vizuri sana wakati wa mchana na mara nyingi huonekana akiwinda mawindo yake nyakati za mchana kitaalamu wanafahamika kama (Diurnals)


Kwa mnyama Chui yeye ana tabia ya kipekee sana ambayo inamfanya awe tofauti na wanyama wengine wote, yeye hupenda kuvamia hapendi kukimbiza mawindo yake tangu akiwa mbali anajitahidi asogelee kwa ukaribu zaidi kisha kufanya uvamizi wa kushtukiza, na mara baada ya kumuua mnyama amuwindae hupanda naye juu ya mti ili kuepuka usumbufu kutoka kwa wanyama wengine kama fisi na simba. Hii ni tabia ya kipekee ambayo inamfanya chui kuwa tofauti na wanyama wengine wote.


#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews #tourism

2 years ago | [YT] | 2

Bantuadventurestv

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Balozi wa Marekani nchini #Tanzania, Mhe. Michael Battle kuhusu mikakati mbalimbali ya kukuza Sekta ya Utalii, pamoja na uhifadhi wa wanyamapori .


Kikao hicho ambacho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Jengo la Mpingo jijini Dar es Salaam, Waziri Kairuki amemuomba Balozi Battle kuhamasisha wawekezaji wakubwa kutoka nchini Marekani kuja nchini Tanzania kuwekeza.


Pia kutokana na idadi ya watalii kuendelea kuongezeka Tanzania kumekuwa na upungufu wa vyumba vya kulala wageni hivyo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya Utalii hasa katika huduma ya malazi kwa kujenga Hoteli, kambi za watalii na huduma za usafiri.


Hata hivyo Balozi Battle amesema nchi yake imekuwa ikifadhili programu mbalimbali nchini kwa kufanya kazi na hifadhi za Serengeti, Ngorongoro, Mkomazi na Ruaha.


Kupitia ushirikiano huu Tanzania na Marekani imezidi kuimarika na hivyo kusaidia kukuza sekta ya Utalii nchini.

Kwa taarifa zaidi usikose kufuatilia YOUTUBE CHANNEL yetu kwa jina BANTUADVENTURES TV na mitandao yetu ya kijamii TWITTER na INSTAGRAM.


#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews #tourism #travel #tanzania

2 years ago | [YT] | 1

Bantuadventurestv

Faru ni miongoni mwa wanyama wa tano ambao ni wakubwa kwa Africa, wanyama wengine ni chui, simba, mbogo na tembo.



Hata hivyo kuna aina tano za faru duniani na kwa Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni Faru mweupe(WHITE RHINO) na fARU Mweusi (BLACK RHINO) na aina nyingine tatu zilizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya Faru ambayo ni Black Rhino ingawa pia kuna White Rhino wanaopatikana #Mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa.


Faru 'mweupe' ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya Tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi, Utofauti wa faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wanavyodhani.


Kwa kawaida Faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja, dume na jike hukutana tu katika msimu wao ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume.


Simba ambao huwinda watoto wa Faru kwa ajili ya kitoweo imesababisha Kutoweka kwa Faru, Pia kumewafanya wanyama hawa wawekewe ulinzi wa masaa 24 na askari wa wanyama pori.


Faru wanauwezo mkubwa sana wa kunusa na kusikia ,pia wanyama hawa hawana kumbukumbu nzuri kama Tembo hivyo hawawezi kulipiza kisasi.


Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea YOUTUBE CHANNEL YETU kwa jina BANTUADVENTURES TV na mitandao ya kijamii.


#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews #tanzania #tourism

2 years ago | [YT] | 2

Bantuadventurestv

#UTALIIWAMAKABILA
Pichani ni nyumba aina ya Tembe zinazo jengwa zaidi na watu wa kabila la Wagogo

#wagogo wanapatikana zaidi katika mkoa wa Dodoma uliopo katikati mwa nchi ya Tanzania na pia ndiyo makao makuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
sukuma mshale mbele kuziona picha zaidi.
#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews

2 years ago | [YT] | 5

Bantuadventurestv

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUTUMIA AKILI BANDIA (AI) KATIKA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE

Wizara ya Maliasili na utalii yaanza kutumi akili bandia katika kutekeleza majukumu yake ili kuleta ufanisi wenye tija katika tafiti za Wanyama na hivi karibuni itaanza kutumia kwenye kuandikisha watalii kutokea nchi wanazotoka hadi kwenye vivutio vya utalii watakavyotembelea.

Haya yamebainika wakati Kamati ya Bunge ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikipokea taarifa ya utekelezaji wa taasisi zilizochini ya wizara ya maliasili na utalii ambazo ni Mradi wa uendelezaji utalii Kusini (REGROW), Chuo cha usimamizi wa wanyamapori Mweka (CAWMM) na Taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi(PWTI).

Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) hutumia akili bandia katika kufanya sensa ya Wanyama waliopo kwenye hifadhi na mapori ya akiba, matumizi ya akili bandia yameleta matokeo chanya hasa katika kupunguza gharama na muda wakati wa kufanya zoezi hilo.

#bantuupdate #bantuadventurestv #bantunews

2 years ago | [YT] | 1