THE GOLD VOICE – Sauti ya Uponyaji na Maadili
Hii ni sauti ya kipekee kutoka kwa Tiba Jacob, mhubiri na mlezi wa ndoa na familia.
Tunagusa maisha kwa mafundisho ya upendo, malezi bora, na thamani ya ujana katika jamii ya sasa.
Jiunge nasi kwa maombi, mafundisho na mwongozo wa maisha ya kiroho na kifamilia.
Fuatilia, shiriki, na kuwa sehemu ya uponyaji wa kizazi hiki.

THE GOLD VOICE – A Voice of Healing and Values
Led by Tiba Jacob, a preacher and family mentor from Tanzania.
This channel shares powerful teachings on love, parenting, and the value of youth in today’s world.
Join us for spiritual insight, prayer, and real-life guidance for marriage and family.
Subscribe, share, and be part of healing a generation.


THE GOLD VOICE

maisha yetu yamejengwa katika misingi ya uzao,na uzao ni sehemu ya ndoa ilohalalishwa na jamii,wazazi na Inayokubalika mbele za Mungu, kuwa na Mpango Mtakatifu wa Kutengeneza Taifa teule la watakatifu hapo ijapo Mungu ataifunga hii Dunia.
Karibu "The Gold Voice "sauti ya maneno yenye thamani ya dhahabu,ujipatie Nusu ya kifahari ukayaishi maisha yenye Tabasamu katika mahusiano na Ndoa yako kiujumla ,Subscribe leo na share pia na mtu mmoja tuiponye ndoa au Mahusiano yake leo.

9 months ago | [YT] | 4

THE GOLD VOICE

Sauti yenye Thamani ya dhahabu inarudi na mguso wa Uponyaji "THE GOLD VOICE ",Hapa ndoa zinaponywa ,Jamii inaangazwa karibu Kwenye safari ya Maarifa Subscribe leo.

9 months ago | [YT] | 4

THE GOLD VOICE

Usipoteze nafasi ,karibu usubscribe hii channel upate maarifa ya kifahari juu ya Mahusiano na Ndoa,share na Mmoja tuiponye ndoa yake/Mahusiano yake.

9 months ago | [YT] | 3

THE GOLD VOICE

Mume ni Tunu kama ilivyo kwa mke,ila yapo mambo yanayoleta maumivu nayo yanakuwa pasua kichwa.
Yafuatayo ni moja ya mambo yanayoweza kukusaidia wewe mke kuishi na mume pasua kichwa katika ndoa yako;
1.kugundua udhaifu wake .
Unapogundua tatizo lako liko wapi mpaka hapo utakuwa umeanza safari ya kuelekea kushinda namna ya kuishi na mume pasua kichwa na kumfanya awe sawa na kukupa thamani yako.
2.kugundua eneo la udhaifu wake.
Unapogundua nafasi au eneo linalouhamasisha udhaifu wake,inakusaidia wewe kama mke kuchukua hatua ya kumsaidia kutoyafikia maeneo hayo kirahisi na itamfanya awe bora zaidi.

3.Gundua anapenda nini kutoka kwako.
Jambo la msingi la kiliishi ni pamoja na kujua vitu anavyopenda kutoka kwako kama mke,unapojua nini anapenda kutoka kwako ,ni fursa sana kwako kujua namna unapaswa kukiwekeza zaidi na kukipa kipaumbele zaidi na zaidi ili kuepusha upasua kichwa huo unao kutesa na kukupa kutomfurahia mumeo.

4.Weka tabia ya kumwambia nini unapenda kutoka kwake.
Kujiweka wazi kwake,nini unakipenda kutoka kwake itampa nafasi ya yeye kujua kuwa ana vitu,ana mambo ambayo yanayokufanya wewe uyapende na kumpenda yeye mwenyewe.

Haya ni moja ya mengi yanayokuwezesha wewe kuishi na kumbadili mume pasua kichwa awe na mabadiliko chanya na kuwa mume pendwa wa mke wake.

#Mahusiano #Ndoa #Mapenzi #Nakupenda #Mckakatiba.

11 months ago | [YT] | 2

THE GOLD VOICE

Fikra yakinifu huzaa matunda mengi sana,ila nayo mathnda hayo huwa yakinifu pia,Yesu kristo aliwambia wanafunzi wake ,mimi ni mzabibu nanyi ni matawi,mtu akikaa ndani yangu Nami ndani yake huyo huzaa sana,umegundua kumbe ukikaa ndani ya uyakinifu na utulivu utazaa matunda yanayoendana na Hali ya ufahamu wako ulivyo,nikusihi jambo moja la muhimu,wewe ni mtu muhimu sana,ila umuhimu wako umefichwa katika utulivu na uyakinifu ndani ya Mungu, tulia utapanda thamani pale utakapo gundua kuwa unapaswa kuwa na thamani katika jamii yako,
Je! Wewe ni moja ya watu walio wahi kudharauliwa kwa sababu ya maamuzi au jinsi uluvyo ? Ulifanya nini ulipogundua unadharaulika?
Weka comment yako hapo chini ulifanya nini ili nasi tujifunze kupitia comment yako ili kupanua uwanja mpana wa fikra za watu wanaopitia wakati wa kudharaulika kwa sasa.
Naitwa Mckakatiba-official, ninanyekuletea maarifa tofautitofauti kupitia channel hii ,na kipindi hiki cha[ The Gold Voice ] subscribe na share pia kwawatu wengine ili tuendelee kujifunza namna ya kukabiliana na vipindi tofauti vya maisha ya Familia,malezi na mahusiano ,kwa ushauri zaidi
What'sApp no 0786876125.

1 year ago | [YT] | 4

THE GOLD VOICE

Uchungu wa moyo wako mwambie Mungu pekee utapona,ila ukitaka maumivu makali yenye kukuuma zaidi,na kuongeza Machungu usoyatarajia kwa wingi zaidi,waambie watu nini kina kuumiza moyo.
Jambo ambalo ulijisahau ni kwamba mara nyingi ubinadamu tunatofautiana,Kuna mtu hapendi tu kumuona mtu mwingine Ana furaha Ana ishi maisha yake Safi hii inamuuma sana mtu asopenda watu wengine kuwa na maisha yoa na kuyafurahia.
Sasa wewe unapojipeleka kumueleza kinachoumiza moyo wako anakukumbatia ,anajiliza ,anajitilia huruma usoni mwake ili Hali amefurahi sana kuipata fursa ya kuitimiza furaha ya kukuongezea maumivi.
Hii inaitwa huruma ilobeba roho mbaya ndani yake,ni ushetani ulojificha ndani ya uso wenye huruma.
Mara nyingi watu kama hao,kujua Nia Yao huwa ni ngumu sana,mpaka uwe mdukuzi wa ulimwengu wa hisia za rohoni ,utagundua huyu ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Sasa jambo la kufanya ni nini ukimgundua mtu wa aina hiyo,mshukuru Mungu, isamehe nafsi yako,halafu jinong'oneze sipaswi kurudia kumkabidhi mtu maumivu ya moyoni.
Hii itakupa dawa ya kukuponya na utaipata Kinga ya kuuganga moyo wako.


Karibu kwenye channel yangu hii ya Mckakatiba-official [The Gold Voice ]
Tushirikiane kuifanya jamii itambue bado inaweza kuwa kwenye ubora kuliko awali.
Subscribe, share, comment .
Niwekee comment yako hapo chini ushawahi kuumia tena ukaumia baada ya kumwambia mtu maumivu yako ???
Karibu tujifunzi kupitia comment yako hapo chini.

1 year ago (edited) | [YT] | 3

THE GOLD VOICE

Katika maisha tunajumuika ili kuzishinda changamoto,tunagawana majukumu kuukomboa wakati,

1 year ago | [YT] | 3

THE GOLD VOICE

Bibie anavyosubiri kipenga cha Mckakatiba-official awape watu vitu vitamu

1 year ago | [YT] | 2

THE GOLD VOICE

Unapokuwa Nami ukumbini ,kila hatua ni surprise to cheki mtoto wa watu anavyobadili pozi hatua kwa hatua.

1 year ago | [YT] | 1

THE GOLD VOICE

Karibu Katika uwanja wetu ,hapa tutacheza namba zote zitakazo kufanya ujione mfalme malkia, Nimedhamilia kukonga mioyo yenu wapenzi ,@Mckakatiba-official [The Gold Voice ]

1 year ago (edited) | [YT] | 1