KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

Football โšฝ for fan
Mpira burudani


KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

๐Ÿ—ฃ๏ธ Miguel Gamondi asema ukweli kabla ya mchezo wa kesho!

Kocha wa Tanzania Taifa Stars, Miguel Gamondi, amezungumza kwa uwazi kuelekea mchezo wa AFCON 2025 dhidi ya Tunisia ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ

โ€œNilisikia swali la mwandishi kwamba tukifungwa nawakasirikia wachezajiโ€ฆ hapana. Mpira ni mchezo wa makosa, lazima ufanye makosa ndipo uwe bora zaidi. Naipenda kazi yangu na nawapenda wachezaji wangu, lakini wakati mwingine lazima tuwe wakweli. Angalia nafasi ya Tanzania kwenye viwango vya FIFA na CAF bado hatupo mahali pa kujilinganisha na wengine.โ€

Gamondi ameongeza:

โ€œSamatta anaweza kuanza au akaanzia benchi. Kwangu, wachezaji wote wako sawa. Hii ni timu ya taifa. Kucheza ligi kubwa Ulaya pekee hakumaanishi lazima uanze.โ€

4 weeks ago | [YT] | 6

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

FAR RABAT NA AL AHLY WANASHUKURU KUWA KUNDI RAHISI MAANA NDIO WANAOVUKA.

Ukiangalia kundi lilivyo unaona kabisa FAR Rabat na Al Ahly ndio wanakundi Rahisi hapa ndio wanaovuka.

Maana Al Ahly na JS Kabylie watachukua sita zote za Kabylie huku Al Ahly atachukua na sita za Yanga,,, Kisha Yanga yeye atachukua moja tu ya JS Kabylie.

1 month ago | [YT] | 1

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

๐Ÿ”ฅ FULL TIME โ€“ International Friendly
Kenya ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช 0 โ€“ 8 Senegal ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ

Senegal wameonyesha ubora wao wa hali ya juu katika mchezo wa kirafiki, wakitumia kila nafasi kwa ufanisi na kuudhibiti mchezo mwanzo hadi mwisho.

Magoli:
โšฝ๏ธ 10โ€™ โ€“ Jackson
โšฝ๏ธ 13โ€™ โ€“ Diouf
โšฝ๏ธ 16โ€™ โ€“ Jackson
โšฝ๏ธ 18โ€™ โ€“ Manรฉ
โšฝ๏ธ 32โ€™ โ€“ Manรฉ (Pen)
โšฝ๏ธ 36โ€™ โ€“ Manรฉ
โšฝ๏ธ 49โ€™ โ€“ Mbaye
โšฝ๏ธ 81โ€™ โ€“ Ndiaye (Pen)

Senegal waliingia kwa kasi na kutengeneza presha isiyokatika, huku Kenya wakipata changamoto kuhimili mashambulizi mfululizo.

๐Ÿ“Œ Matokeo haya yanawapa Senegal motisha zaidi kuelekea michuano ijayo, huku Kenya wakibakiwa na masomo muhimu ya kurekebisha kabla ya mechi zinazofuata.

2 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

๐…๐”๐‹๐‹ ๐“๐ˆ๐Œ๐„ : NBC Premier League ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

JKT TANZANIA FC 1๏ธโƒฃโž–๏ธ2๏ธโƒฃ SIMBA SPORTS CLUB
โšฝ๏ธ 60" Songo โšฝ๏ธ 64" Nangu
โšฝ๏ธ 77" Sowah

2 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

Half time: Mchezo kati ya Seychelles ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡จ na Ivory Coast ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ kipindi cha kwanza kimemazilika Ivory Coast wakiwa mbele kwa goli 4๏ธโƒฃโž–0๏ธโƒฃ

magoli yamefungwa na I. Sangarรฉ 7' (P) E. Agbadou 17' O. Diakitรฉ 32' E. Guessand 39'

Lakini fundi wa Mpira Pacome Zouzou bado hajaingia kambani kama anavyofanyaga huku tanzania tuendelee kusubiri kipindi cha pili huenda akafunga ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™Œ๐Ÿป

3 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

๐— ๐—” ๐—ก ๐—ฆ ๐—› ๐—” ๐—Ÿ ๐—˜ ๐—˜ ๐—” ๐—จ ๐—ช ๐—” ๐—”๐Ÿคฉ๐Ÿ”Ÿ๐Ÿฆ

3 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

Kesho J'Nne Oct 07, 2025 kinapigwa pale meja jeneral isamuyo
Ni Simba SC Tanzania dhidi ya AL HILAL omdumani
Ni match ya kirafiki na itakuwa (closed door)
Ni mechi maalumu kwa ajili ya benchi jipya la ufundi kuangalia wachezaji wao na kufanya tathmini za kiufundi.

3 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

Pale AZAM TV kwa sasa kuna uhaba wa Watangazaji wazuri wa mpira. Kuna watu wanalazimishwa watangaze lakini hawana radha kabisa.

Kwa sasa Azam TV watangazaji wa maana ni:

1. Gharib Mzinga
2. Ayoub Hinjo
3. Salum Iddi Kidedea
4. Gwalugano Mwakalobo

Inatakiwa wazalishe vijana wapya au waende kwenye media zingine wakapore watangazaji wengine mfano Seif Bongi pale ZBC 2 na Nazareth Upete pale TBC.

Hawa akina Pascal Kabombe, Hassan Mvula, Alwatan Ngoda wabaki kwenye majukumu mengine.

Haiwezekani unakuta Game kali, alafu Mtangazaji amepoa kinyama ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

3 months ago | [YT] | 4

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

๐Ÿ—ฃ๏ธ๐Ÿ”ฅ *"Tukiwa wakweli kabisa, uwezo wa mchezaji mmoja mmoja upo chini sana. Wanapaswa kurudi uwanjani kufanya mazoezi zaidi ili kurekebisha hali hii na kuweza kushindana na wengine."*
โ€” *Kocha Hemed Suleiman Morocco*, Kocha wa muda Simba SC ๐Ÿฆ

๐Ÿ“Œ Kauli ya ukweli inayogusa msingi wa ushindani wa kweli ๐Ÿ’ฏ
Soka ni zaidi ya majina, ni maandalizi, nidhamu na ubora binafsi uwanjani.

๐Ÿ“ฃ *Je, unakubaliana na Kocha Morocco?*
๐Ÿ‘‡ Acha maoni yako hapa chini!

โค๏ธ *Like | ๐Ÿ’ฌ Comment | ๐Ÿ‘‰ Follow* โ€ช@simbasctanzania255โ€ฌ

3 months ago | [YT] | 0

KEV MSUYA SHOW "SPORTS"

Azam Tv tafuteni watangazaji Professional wa Mpira waliochangamka, hawa mlionao wanatangaza kama wanasoma taarifa ya habari

Yani tunaangalia Mpira kama tunaangalia Tamthilia ya kituruki au mazishi, watangazaji wamepoa kama uji wa mgonjwa๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก

Basi tu hatuna Option ya kuangalia mpira channel nyingine ndiomaana tunawaangalia ila mara 100 mpira wa kusikiliza youtube au kwenye redio kuliko kuangalia mechi zenu

3 months ago | [YT] | 0