Yuboxtv ni televisheni ya mtandaoni ambayo inajihusisha na kuripoti matukio yote ndani na nje ya mipaka ya Tanzania sanjari na uzalishaji wa vipindi mbalimbali vya kijamii, hususani vinavyohusu vijana. Kila siku kupitia mitandao ya kijamii Instagram, Twitter na Facebook.
Yuboxtv inalenga kubadilisha mtazamo wa jamii kwa kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha.


Yuboxtv

TANZIA
Aliyekuwa, Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika na Mbunge wa Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile ameaga dunia usiku wa kuamkia leo nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dkt. Ndugulile alichaguliwa nafasi hiyo ya Ukurugenzi Agosti 27, mwaka huu, huku akitarajia kuanza kutumikia wadhifa huo mwezi Februari, 2025.

1 year ago | [YT] | 4

Yuboxtv

RAIS DKT. SAMIA ATEMBELEA GHOROFA LILILO POROMOKA KARIAKOO-DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ,mapema Novemba 20, 2024 amekagua eneo ilipotokea ajali ya kuporomoka kwa ghorofa katika kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
 
Aidha, Rais Dkt. Samia ambaye aliongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amepata wasaaa wa kuwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

#Raissamia #ikulumawasiliano

1 year ago | [YT] | 4

Yuboxtv

Tumetoka kwenye #AFL kutokana na goli la ugenini. #WenyeNchi #NguvuMoja

2 years ago | [YT] | 9