CoP DODOMA CITY CHURCH

A center of Transforming and Equipping Christians to impact their societies by Kingdom values and Principles.
Dodoma City, Tanzania.


CoP DODOMA CITY CHURCH

SOMO: FUATILIA UJUMBE WA INJILI

Ukimkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako, safari haiishii kwenye kuokoka tu. Unahitaji kuielewa Injili, kuishi ndani yake na kuifikisha kwa wengine.

Dhambi ilimtenga mwanadamu na Mungu, lakini kupitia kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, njia ya upatanisho imefunguliwa. Kwa kumwamini Kristo, tunapata uhusiano mpya na Mungu na uzima wa milele.

Injili si ujumbe wa kusikia na kuusahau; ni Nguvu ya Mungu iletayo wokovu kwa kila aaminiye. (Warumi 1:16)

Kwa hiyo, mwamini aliyeipokea Injili anaitwa kuendelea kushikamana nayo, kuishi kulingana nayo na kuwa balozi wa Kristo, akiwaalika wengine wapatanishwe na Mungu.

Swali la kutafakari: Je, baada ya kuipokea Injili, unawafikishia wengine Habari Njema ya Yesu Kristo?

📖 1 Wakorintho 15:1-3; 2 Wakorintho 5:18-20

#FuatiliaUjumbeWaInjili #Injili #YesuKristo #NenoLaMungu #HabariNjema #Wokovu #Imani #Evangelism #TheChurchOfPentecost #DodomaCityChurch

1 month ago | [YT] | 8

CoP DODOMA CITY CHURCH

TUNAANZA NA BWANA NA TUNAMALIZA NA BWANA KWA USHINDI.
Ungana nasi kwa Njia ya Simu Kila siku ya Jumatatu kwa Maombi Maalumu ya Kuimauru Wiki Mpya na Kuanza na Bwana kwa Uweza na Nguvu zake.
#maombi

1 month ago | [YT] | 3