Reality of God's Grace Ministries International.
Dar es Salaam, Tanzania.
[The Ministry of God under His humble servants Apostle ASTTON and Prophet ALLEN] (Twins brothers)
The Reality of God's Grace, abbreviated as "RGG", is the God given mandate, ministry and mission to the World.
This is the New covenant Ministry, built on the foundation of Jesus Christ, "We are Christ centered, Christ minded and Christ alike."
RGG is the Ministry that inspires ,raises and generates men and women in the FAITH as an army of mighty people of faith- through the Holy Spirit and Sound teaching (doctrine), "the revelation of the Word and manifestation of the Spirit (power)."
We are always believing, growing building up, learning,leading,following and looking unto Christ Jesus,the author and finisher of our Faith.
Connect with Us.
aprggtz@gmail.com
wa.me/qr/X67PX5KBKOARO1
+255 628 105 274 WhatsApp
+255 655 008 730 WhatsApp
"The Grace of God is Sufficient for us"
RGG Ministries International
RGG Channel +255
NDOA NI NINI?
+255628105274
aprggtz@gmail.com
Na, Apostle ASTTON.
1 week ago | [YT] | 11
View 0 replies
RGG Channel +255
40 DAYS OF FASTING.
DAY 24 | WAZAZI NA WALEZI.
- Tunao wazazi na walezi wakimwili na wakiroho ambao ni Mungu ametupa. Watu hawa ni wa muhimu.
OMBA;
- Natamka afya njema, uzima tele, furaha, upendo, amani na ulinzi wa kiungu wa wazazi na walezi wangu katika Jina la Yesu.
- Nawaombea moyo wa kumcha Mungu, ibada, neema ya wokovu na maisha marefu ya ushindi na mafanikio tele katika Jina la Yesu. Amen!
[Wakumbuke Kwa zawadi, fedha na kuhumia mahitaji ya wazazi wako]
Maandiko ya maombi;
Kutoka 20:12 | Kumbukumbu la torati 5:16 | Mithali 23:22 | Mithali 3:1-2 |
*2026 - Possession & Dominion*
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
1 week ago | [YT] | 5
View 0 replies
RGG Channel +255
1st February 2026.
The HOMOLEGEO.
"Believe to Receive"
NAMCHA MUNGU.
"Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu."
- 2 Wakorintho 7:1
Ucha Mungu ni hali ya kumheshimu, kumpenda, kumtii na kumweka Mungu kwanza katika maisha yako, kwa hofu takatifu (si woga wa kuogopa adhabu, bali heshima ya ndani). Mcha Mungu anafahamu wazi kwamba hakuna namna anaweza kujificha mbele ya macho ya Mungu.
Kila mwamini ni muhimu kuwa na roho ya ucha Mungu na kumcha kwa kumaanisha. Usifanye vitu kwa kuanza kuangalia watu au mazingira bali kumwangalia Mungu kwanza. Ucha Mungu si woga wa kumkimbia Mungu, bali ni heshima inayokufanya ushindwe kumkosea Mungu hata ukiwa peke yako.
AMINI KUPOKEA;
Naamini mimi ni mcha Mungu, nina mcha katika roho na kweli, sita kaidi sauti yake, amri yake na neno lake. Nina dumu katika haki na utakatifu wa kweli nikijua Mungu ndiyo kila kitu kwangu, na wakati wote nina zingatia mapenzi yake katika Jina la Yesu. Amen!
Maandiko ya msisitizo;
Isaya 11:2 | Mhubiri 12:3 | Mithali 10:27 |
MIMI NI MCHA MUNGU.
Apostle ASTTON.
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
1 week ago | [YT] | 12
View 1 reply
RGG Channel +255
40 DAYS OF FASTING.
DAY 21 | ROHO 7 ZA BWANA.
Leo tutafakari nakuomba juu ya Roho Saba za Bwana (udhihirisho na ukamilifu wa Mungu kama Roho) kwenye maisha yetu. Tuzidi kujawa na kudhihirisha hekima, ucha Mungu, maarifa, uweza, fahamu, shauri na ubwana wa Bwana Yesu maishani mwetu.
(Omba na Kutafakari maandiko haya)
Maandiko ya Maombi;
Isaya 11:2 | Ufunuo 1:4 | 2 Timotheo 1:7 | Wakolosai 1:9
2026 - Possession & Dominion.
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
1 week ago | [YT] | 6
View 0 replies
RGG Channel +255
31st January 2026.
The HOMOLEGEO.
"Belive to Receive"
NABURUDIKA.
"Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo."
- Philemon 1:20.
Tuna burudishwa katika Kristo Yesu, waamini tunayo raha na furaha ambayo haipatikani kwa mwingine yeyote ispokuwa Kristo. Ndiyo maana hatukamilishwi kwa kuoa au kuolewa, kupata kiwango fulani cha elimu au fedha na mali, bali tumekamilishwa katika Kristo.
Yatazame maisha yako mapya kama maisha ya raha, furaha na sio taabu, huzuni na uchungu. Tuna burudika katika Kristo kwasababu tumejawa Roho, Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
AMINI KUPOKEA;
Naamini katika burudiko la kiroho katika Kristo Yesu. Hakuna taabu, huzuni, masikitiko, uchungu wala maumivu yatakaa ndani yangu. Nimejawa amani, furaha, raha ya uzima wa milele na uwepo wa Mungu kwangu katika Jina la Yesu. Amen!
Maandiko ya Msisitizo;
Warumi 14:17-19 | Waefeso 5:18.
NINA BURUDIKA.
Apostle ASTTON.
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
1 week ago | [YT] | 8
View 0 replies
RGG Channel +255
40 DAYS OF FASTING.
DAY 20 | TUNDA LA ROHO.
Tunda la roho ni ushahidi wa uwepo wa Roho wa Mungu ndani yetu, ushahidi kwamba tume okolewa na sisi ni sura na mfano wa Yehova. Kila mmoja mwombe Mungu Tunda la Roho lidhihirike na kuwa dhahiri maishani mwako. Uwe mtu wa upendo, usamehe, uwe na utu wema, kiasi, upole, uvumilivu na fadhili.
Maandiko ya maombi;
Wagalatia 5:22 | Waefeso 5:9 | 1 Wakorintho 13:1-13.
2026 - Possession & Dominion
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
1 week ago | [YT] | 1
View 0 replies
RGG Channel +255
30th January 2026
The HOMOLEGEO.
"Belive to Receive"
MIMI NI MWANA WA NURU.
"Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru."
- Yohana 12:36.
Mwana wa nuru ni nuru, hivyo ndivyo waamini (tuliookoka) tulivyo. Tumepata nuru na tumefanyika nuru katika Yesu Kristo. Mwana wa Nuru maana yake - unatokana na nuru.
Kuna giza la kimwili na giza la kiroho, mwana wa Mungu haupaswi kumilikiwa au kutawaliwa na giza (uovu, ibilisi). Sisi ni nuru inayo angaza ambayo giza halita iweza. Yesu alisema 'Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima'. Maana yake sisi ni kitu cha kuonenaka kisichoweza kufichika.
AMINI KUPOKEA;
Nina amini mimi ni nuru, natokana na nuru. Kupitia mimi kila kinachopaswa kuonekana kina onekana, nina na angaza rohoni mpaka mwili. Matendo yangu, maneno yangu na mawazo yangu ni ya nuru tu wala hakutakuwamo giza ndani yake katika Jina la Yesu. Amen!
Maandiko ya msisitizo;
Yohana 1:4-5 | 1 Yohana 1:5
MIMI NI NURU.
Apostle ASTTON.
'Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
2 weeks ago | [YT] | 11
View 0 replies
RGG Channel +255
40 DAYS OF FASTING.
DAY 19 | WALIORUDI NYUMA.
Haya ni maombi ya kurejeza wengine, wapo watu ambao walikuwa wamesimama vizuri kiroho, lakini Sasa wamerudi nyuma, walikuwa waamini wazuri, watumishi wazuri, changamoto za kidunia na mashambulizi ya shetani yamewapata wakishindwa kustahimili wamerudi nyuma. Mungu anawapenda na anataka wamrudie (Toba ya kweli) wasimame wasi anguke tena. Tuwaombee moyo wa toba, unyenyekevu na kuitikia sauti ya Mungu.
Maandiko ya maombi;
Yakobo 5:19-20 | Yakobo 5:15-16 | Matendo 3:19.
2026 - Possession & Dominion
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
2 weeks ago | [YT] | 5
View 0 replies
RGG Channel +255
29th January 2026.
The HOMOLEGEO.
"Believe to Receive"
NAKAZA MWENDO.
"nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu."
- Wafilipi 3:14.
Paulo mtume, aliweka wazi aliposema "Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. Wakati wote lazima uwe mtu wa kuendelea mbele, usikubali kabisa kurudi nyuma.
Paulo aliendelea kusema; "Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;". Songa mbele usigeuke nyuma, woko uliona, hatima yako, kusudi lako na maono uliyonayo jifunze kukaza mwendo katika Kristo Yesu.
AMINI KUPOKEA;
Naamini katika kasi ya kiungu na uelekeo sahihi. Sitatazama nyuma, nina songa mbele, nina endelea mbele, sitapoa nina zidi kuwa moto, sitaacha yale ambayo Kristo amenipatia. Nina kwenda Kwa kasi, kwa usahihi na mafanikio makubwa katika Jina la Yesu. Amen!
Maandiko ya msisitizo;
Wafilipi 3:1-21 | Wagalatia 5:7
NAPIGA MBIO.
Apostle ASTTON.
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
2 weeks ago | [YT] | 6
View 0 replies
RGG Channel +255
40 DAYS OF FASTING.
DAY 18 | WALIOKO MAGEREZANI.
Leo tuombe kwaajili ya watu wote wake Kwa waume walikoko magerezani, wengine wamesha hukumiwa mahakamani na wengine bado. Wapo ambao wamesingiziwa makosa na wengine ni kweli wamefanya. Tuombe kwaajili yao, wapate nuru ya wokovu, wakutane na pendo la Mungu, wapate ushindi, wapate msamaha, wawe watu wema, wenye afya njema, wamtumikie Mungu. Leo Mungu anaingilia kati watu walioko magerezani, tunao wajua na tusio wajua.
Maandiko ya maombi;
Matendo 12:5-11 | Matendo 16:25-31. | Wafilipi 4:6.
2026 - Possession & Dominion.
"Neema ya Mungu Inatutosha"
RGG Ministries International.
2 weeks ago | [YT] | 3
View 0 replies
Load more