Babdeo is a channel that broadcasts programs about education, entertainment in the community

Babdeo ni chaneli inayotangaza vipindi kuhusu elimu, burudani katika jamii


BABDEO MILADU

PIERRE LIQUID ASILIMU NA KUWA MUISLAM

Msanii na mchekeshaji Peter maarufu kama Pierre Liquid 45 amesilimu na kutamkishwa Shahada na Sheikh Nurdin Kishki.

Tukio hilo la kusilimishwa limefanyika ndani ya Ofisi ya Sheikh Nurdin Kishki tarehe 25 Novemba 2024.

Pierre amechagua jina la Salum ndilo aliliolipenda kuitwa na kwasasa anaitwa Salum.

Mwenyezi Mungu amjaalie thabit katika Imani yake.

@miladu_tv
#MiladuUpdates #miladutv #babdeoMiladu

4 months ago | [YT] | 270

BABDEO MILADU

MAADHIMISHO YA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W 2024

Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) linapenda kuwataarifu Waislam na Watanzania kwa ujumla kwamba, Maulidi ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W Kitaifa yatasomwa usiku wa Jumapili tarehe 15/09/2024 katika viwanja vya CCM Kalangalala Geita Mjini na kufuatiwa na Baraza la Maulidi litakalofanyika siku ya Jumatatu tarehe 16/09/2024 katika Viwanja hivyo hivyo vya CCM Kalangalala Geita Mjini.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan

Hivyo siku ya Jumatatu tarehe 16/09/2024 itakua siku ya mapumziko ya Maulid. Mheshimiwa Mufti Mkuu wa Tanzania Dr Sheikh Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana @muftitanzaniaofficial, kwa niaba ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania anawatakia Sherehe njema za maadhimisho ya Maulid na mapumziko mema.

Imeandikwa na Alhaji Nuhu Jabir Mruma
Katibu Mkuu

@miladu_tv
#MiladuUpdates #miladutv #babdeoMiladu

7 months ago | [YT] | 221

BABDEO MILADU

*OFISI YA MUFTI ZNZ YACHUKUA HATUA*

Siku kadhaa zilizopita kwenye mitandao ya kijamii ilisambaa video ikiwaonesha vijana waliojinasibisha na Madrasa wakiimba nyimbo zisizo na maadili. Ofisi ya Mufti ilipambana kuwasaka vijana hao na kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhid yao.

Ufafanuzi zaidi kuhusiana na taarifa hii tunaifuatilia kwa undani zaidi na tutaleta mrejesho

@miladu_tv
#MiladuUpdates #miladutv #babdeoMiladu

7 months ago | [YT] | 83

BABDEO MILADU

Kipi bora, kumsalia Mtume au kunywa pombe katika Mji Mtukufu

1 year ago | [YT] | 42

BABDEO MILADU

"Siku nyingi nilitamani niwe katika Uislam, ila muda umewadia. Biblia imetaja Kusujudu mara 66, lakini hakuna Kanisa linasujudu" ------Amber Leibrock

Mpiganaji na Bingwa wa ngumi za mapigano ya MMA Marekani aliesilimu miezi miwili iliyopita.

Subscribe #BabdeoMiladu

miladu_tv
#MiladuUpdates #miladutv #babdeoMiladu

1 year ago | [YT] | 185

BABDEO MILADU

MENGI YASIOJULIKANA KATI YA VITA YA GHAZA
"Waarabu wako upande wa ndugu zao Mayahudi, na Waislam wako upande wa Palestina na walichojichanganya Wapelestina ni kutokujua wao ni Maadui wa Waarabu na Waisrail tokea zama za zama. Wakaacha kabila lao Utamaduni wao wakauvaa Uwarabu na Uyahudi, inahitaji akili na elimu kubwa kuijua Vita hii. Allah inusuru Kudusiy"

Maneno ya Sheikh Anuar Jongo katika page yake ya Facebook akiambatanisha na Video ya wanaosadikika ni Waarabu wakicheza Ngoma za kiasili na Mayahudi.

@miladu_tv
#MiladuUpdates #miladutv #babdeoMiladu

1 year ago | [YT] | 66

BABDEO MILADU

https://youtu.be/poNXbIVS4E0?si=MG36H...

*SHEIKH MZIWANDA AWARIPUA MAASKOFU NA WARAKA WAO*

KWANINI KATOLIKI NA ISIWE MAKANISA MENGINE?

KWANIN WAHIMIZE LIPELEKWE MAKANISANI?

WALITUMIA KIGEZO GANI KUWA WENGI HAWATAKI?

KATIKA UPOTEVU WA MAKONTENA, KANISA KATOLIKI LILIHUSIKA BANDARINI

Subscribe Babdeo Miladu

1 year ago | [YT] | 47

BABDEO MILADU

https://youtu.be/v1qyL1HO_WE


"SERIKALI SASA KUJA NA MFUMO MPYA WA DINI" HATUTAKI DINI MSETO, WAZIRI AKUTANE NA SISI KULINDA AMANI
------Sheikh Mussa Kundecha


Subscribe Babdeo Miladu

1 year ago | [YT] | 18

BABDEO MILADU

INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIU

Aliewahi kuwa Imamu Msikiti wa Idrissa Sheikh Ali Baasaleh amefariki leo Juli,30 katika Hospitali ya Agakhan.

M/Mungu amsamehe alipokosea na alinawirishe Kaburi lake

1 year ago | [YT] | 379

BABDEO MILADU

https://youtu.be/o6XeIsRJdlA

KEJELI ZA MH.LEMA NA VIONGOZI WA DINI KUDAI KULA NAO KITIMOTO | MKATABA WA DP WORLD NA UDINI | MH RAIS KUITWA MVAA USHUNGI.
-------Sheikh Muhammad Iddi



Subscribe Babdeo Miladu

1 year ago | [YT] | 5