TRT Afrika Swahili

Afrika kama ilivyo


TRT Afrika Swahili

Ujumbe wa kimataifa wa mshikamano unamiminika baada ya ndege ya mizigo ya kijeshi ya Uturuki iliyokuwa na wanajeshi 20 kuanguka kwenye mpaka wa Azerbaijan na Georgia mnamo Novemba 11.

Rais Erdogan wa Uturuki ametoa rambirambi kwa familia za mashahidi na kuapa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

2 months ago | [YT] | 2

TRT Afrika Swahili

Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 1972.

Hata hivyo, Julius Kambarage Nyerere na Rashid Mfaume Kawawa waliwahi kuhudumu nafasi hiyo wakati nchi hiyo ikijulikana kama Tanganyika kabla ya cheo hicho kufutwa kati ya Novemba 1964 na Februari 1972.

Nani atakuwa mrithi wa Majaliwa Kassim Majaliwa?

2 months ago | [YT] | 10

TRT Afrika Swahili

Tangu Okotoba 1, vikosi vya Israel vimewakamata wanaharakati wa kimataifa 223 waliokuwa kwenye msafara wa Sumud Flotilla uliokuwa njiani kuelekea Gaza. Licha ya kuzuia msafara huo mara 20 kinyume cha sheria, meli moja — Mikeno — ilifanikiwa kukwepa mtego na kufika maeneo ya bahari ya Palestina

3 months ago | [YT] | 1

TRT Afrika Swahili

Sikiliza muhtasari wetu wa habari ya siku ya Agosti 4.

🎧 Sikiliza hapa: trt.global/afrika-swahili/audio/62aa84efde47

5 months ago | [YT] | 0

TRT Afrika Swahili

Wanajeshi wa Uingereza walioko Kenya kwa mafunzo chini ya mpango wa BATUK kwa zaidi ya nusu karne wamehusishwa na madai mazito ya ubakaji, mauaji, na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wanawake na watoto wanaoishi karibu na kambi zao.

Ntilaren Supuko na wengine wanasimulia jinsi walivyodhulumiwa kingono na wanajeshi wa Uingereza.

Aidha, kuna ongezeko la watoto machotara waliotelekezwa, ambao inadaiwa ni watoto wa wanajeshi hao.

Badala ya kuimarisha amani, wanajeshi hawa wamegeuka kuwa mwiba mchungu.

8 months ago | [YT] | 2

TRT Afrika Swahili

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ndiyo nchi inayozalisha madini ya kobalti kwa wingi duniani, yaliyo muhimu kwenye mabetri ya gari yanayotumia umeme.

Na huku kukiwa na mapigano na bei yake kushuka sana, nchi hiyo imesitishwa usafirishwaji wa kobalti nje ya nchi - hatua ambayo inaweza kuathiri pakubwa soko la dunia.

Hizi ni nchi tano ambazo madini ya kobalti yanapatikana kwa wingi katika mataifa yao.

10 months ago | [YT] | 5

TRT Afrika Swahili

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo la kulifunga Shirika la Habari la Sauti ya Marekano-VOA linalofadhiliwa na serikali.

Trump amelishutumu Shirika hilo kuwa "linampinga yeye" na "lina msimamo mkali."

Ikulu ya Marekani imesema agizo hilo "litahakikisha walipa kodi hawako kwenye ndoano tena ya propaganda kali."

Hata hivyo, uamuzi huo unaathiri maelfu ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa huduma yao kwa Shirika hilo katika sehemu tofauti barani Afrika na katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Marekani.

10 months ago | [YT] | 4

TRT Afrika Swahili

Nyegere ni mnyama wa kupendeza sana, anayejulikana kwa ujasiri wake wa kipekee na uwezo wa kupigana na wanyama wakubwa kama simba, huku pia akijivunia ngozi yake ngumu na uwezo wa kula nyoka hatari.

1 year ago | [YT] | 4

TRT Afrika Swahili

Afrika imebarikiwa na aina mbalimbali ya ndege, wengine wakivutia kutokana na muonekano wao. Miongoni mwa ndege hao ni korongo ambae anapatikana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki, huku Uganda wakimtumia kama nembo ya taifa.

Je, unajua kama ndege huyu anakuwa na wenza mmoja tu maishani mwake?

1 year ago | [YT] | 14

TRT Afrika Swahili

Je, unajua?

Fungo wa Afrika sio tu wanyama wa porini bali pia wana mchango mkubwa katika mazingira!

Kuanzia harufu maalum wanayoitoa inayotumika kutengeneza manukato, hadi kusafisha mazingira kwa kula mizoga, na kusaidia mimea kukua kupitia usambazaji wa mbegu.

Wanyama hawa wa usiku husaidia kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao na wanaheshimiwa sana kwenye tamaduni za Kiafrika.

Fahamu zaidi kuhusu wanyama hawa wenye hadhi ya kipekee!

1 year ago | [YT] | 8