NUMBER ONE Media House Channel for Breaking News, Entertainment News. Get to know what is happening in Tanzania through GLOBAL TV ONLINE.


Global TV Online

❀️❀️

1 day ago | [YT] | 1,278

Global TV Online

TRA YAFANIKIWA KUVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO KWA MIEZI 9 MFULULIZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa miezi tisa mfululizo, tangu kuanzishwa kwake. Hii ni kutokana na ushirikiano mkubwa uliofanywa na wanahabari na wahariri wa vyombo vya habari, ambao wamekuwa wakitumika kama daraja la kuhamasisha wananchi, hasa walipa kodi, kuhusu umuhimu wa kudai risiti wanaponunua bidhaa na kutoa risiti wanapouza bidhaa zao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA makao Makuu Richard Kayombo, wakati akitoa salamu za Kamishina Mkuu wa TRA alipohudhuria mkutano Mkuu maalumu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wa kuchagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na viongozi wa kamati ya utendaji ya Jukwaa hilo uliofanyika Aprili 5, 2025, mjini Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Kayombo alisema kwamba mafanikio haya yanatokana na ushirikiano mkubwa kati ya TRA na wahariri, ambapo wamekuwa wakishirikiana pale panapokuwa na changamoto au maswali, kwa kutoa ufafanuzi au taarifa muhimu kwa jamii. Aliongeza kuwa mafanikio haya yamewezesha TRA kuongeza wigo wa ushirikiano na vyombo vya habari, hivyo kufanikisha malengo ya ukusanyaji mapato kwa miezi tisa mfululizo.

"TRA inajivunia mafanikio haya ambayo yameletwa na juhudi za pamoja. Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano wa karibu kati ya serikali, vyombo vya habari, na jamii. Hatua hii pia inachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya miundombinu ya usafiri, hasa barabara na njia za usafiri wa ndege ambazo awali zilikuwa hazipo," alisema Kayombo.

Katika mkutano huo, Kayombo pia aliwashukuru wahariri kwa mchango wao mkubwa katika kuchochea umoja baina ya walipa kodi na TRA, na aliwahimiza kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti, ili kuhakikisha kuwa malengo ya ukusanyaji mapato yanaendelea kufikiwa.

Afisa Uhusiano Mkuu kutoka TRA, Rachel Nkundai, alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kulipa kodi, kwani ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha maendeleo endelevu kwa taifa. Alipongeza wahariri kwa juhudi zao za kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya kodi, na aliwahakikishia kuwa TRA itaendelea kushirikiana nao ili kuboresha sekta ya kodi nchini.

Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma, Nicodemus Mwakilembe, alitoa pongezi kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kuendesha uchaguzi kwa uhuru na haki. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha umoja ndani ya jukwaa hilo ili kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana.

Mkutano huu maalumu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliofanyika Ruvuma, unatarajiwa kuchochea ongezeko la mapato kwa mwezi ujao, huku Kayombo akisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kushirikiana na TRA na kudai risiti ili kuchangia maendeleo ya mkoa wa Ruvuma na taifa kwa ujumla.

Huu ni mfano mwingine wa ushirikiano wa kipekee kati ya vyombo vya habari na serikali, ambao umezaa matunda ya mafanikio ya kiuchumi, na inaonekana kama njia ya kuhakikisha kuwa malengo ya ukusanyaji mapato yanafikiwa kwa manufaa ya wote.

1 day ago | [YT] | 39

Global TV Online

Kitu gani kilikupa umaarufu shuleniπŸ“š

1 day ago | [YT] | 80

Global TV Online

πŸ€”πŸ€”KWANINI BADO UNA NUMBER ZA EX WAKO KWENYE SIMU YAKO??πŸ€”

1 day ago | [YT] | 113

Global TV Online

KITOTO CHA YANGA KIMEPITA NA SHATI LA BABA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ I CAN’T WAIT KESHO KUIONA πŒπ€π’π‡π€π“πˆ πƒπ€π˜ KMC PALE

JAMBO LIMESHAKUWA LA MOTOOOOπŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½

1 day ago | [YT] | 85

Global TV Online

Minister of Enjoyment πŸ˜„ @bakarimahundu01

1 day ago | [YT] | 162

Global TV Online

TRA WAPONGEZA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI - BALILE ASHINDA UCHAGUZI TEF

Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF limefanya uchaguzi mkuu wa kumchaguwa mwenyekiti na Kamati tendaji kama ilivyoada katika kutekeleza katiba ya chama hicho ambapo Deodatus Balile amechaguliwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa jukwaa hilo hilo kwa mara nyingine

Uchaguzi huo umefanyika wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma katika Ukumbi wa Bombambili ukihusisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao wameshiriki uchaguzi huo

Deodatus Balile ambaye hapo awali amekuwa kiongozi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa TEF kwa miaka mitano kwa mara nyingine tena amepewa dhamana ya kuendelea Kuongoza kwa nafasi hiyo ya Mwenyekiti na ameahidi kufanya kazi kwa ubora uleule katika kulinda maslahiya wanahabari na kuleta mabadiliko katika Tasnia ya habari

Naye mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) Edwin Soko amepongeza na amesema kuwa inaonesha dhahiri umoja na utulivu ndani ya TEF hivyo MISA TAN itaendelea kushirikiana kwa ukaribu na TEF kakika kulinda na kutetea uhuru kwa vyombo vya habari na wanahabari katika mazingira salama

Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) Richard Kayombo amepongeza Vyombo vya habari kuwa vimekuwa ni kichocheo kikubwa katika mafanikio ya ukusanyaji wa mapato Chini

Akizungumza katika Mkutano mkuu wa jukwaa la Wahariri Tanzania TEF uliofanyika katika ukumbi wa Bombambili songea amesema ushirikiano uliopo kati ya TRA na Wahariri wa vyombo vya habari umechangia kwa kiasi kikubwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa miezi tisa mfulizo

Richard Kayombo akitoa Salamu za Kamishna Mkuu wa TRA katika Mkutano huo wa uchaguzi wa viongozi wa TEF amesema kuwa wanahabari wamekuwa daraja muhimu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutoa risiti na kudai risiti pamoja na kulipa kodi

2 days ago (edited) | [YT] | 64

Global TV Online

❀️❀️GIANT MTOTO WA AJABU https://youtu.be/_7AoLuEWBiY

2 days ago | [YT] | 19

Global TV Online

πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯UNAFUATILIA GLOBAL TV UKIWA WAPI?πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

2 days ago | [YT] | 78

Global TV Online

POLICE FAMILY DAY❀️❀️

2 days ago | [YT] | 133