Huduma yangu ni kumtukuza Mungu kwa kuinua maneno ya nyimbo zetu kuu za kikiristo. Ingawa ninatumia usaidizi wa AI katika kuandaa nyimbo hizi, kiini cha mradi huu ni ushairi wa zamani na wa kudumu wa nyimbo hizi unaomhimidi Kristo.


Tenzi za Rohoni

https://youtu.be/INknW5AdwWc
Ulipomuamini yesu, Ilikua siku kuu ambayo hauwezi sahau kamwe . Dhambi zako zilisamehewa , Mizigo zako zilitwuliwa , ulifanyika mwana wa Mungu na mridhi pamoja na Kristo Yesu, ulifanyika Kiumbe kipya , na ya kale yalipita . Kwanziq hapo , yesu akawa pendo lako kuu

5 months ago | [YT] | 2

Tenzi za Rohoni

Wimbo huu unatufunza maneno haya
1.Uhakika wa Imani kutoka Kwa Neno la mungu: Furaha inayotokana na kupata ahadi binafsi katika "Chuoni mwake" (Biblia) kwamba Yesu anampenda .

Urejesho : Hata wale Mungu aliowachagua katikabyesu wanapotangatanga mbali, upendo wa Mungu unabaki thabiti na unawavuta wamrejee Yeye kwa huruma.

Dhabihu ya Upendo : Huu ni msingi wa imani ya Kikristo—imani kwamba upendo wa Yesu ulithibitishwa kupitia kifo chake msalabani kwa ajili ya wokovu.

Ushindi na Amani : Imani inatajwa kama chanzo cha faraja na nguvu inayoweza kufukuza giza la kiroho au "adui" (shetani) kupitia furaha ya kumwamini Kristo.

6 months ago | [YT] | 7

Tenzi za Rohoni

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
John 3:16
Upendo wa mungu Kwa wanadamu unadhihirika wazi kupitia Kwa mwanawe yesu Kristo ambaye alijitoa mwenyewe kama dhabihu impendezaye mungu Kwa ajili wale wote wamuaminiae . Tumaini katika Kristo yesu ni njia ya pekee ya kuingia katika wokovu huu mkuu,.

6 months ago (edited) | [YT] | 9