RC SENYAMULE AKAGUA MAANDALIZI YA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE, ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIUNDOMBINU
Na Mwandishi Wetu – Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, leo Julai 8, 2026, ametembelea na kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nanenane vya John Samwel Malecela Nzuguni, Jijini Dodoma.
Baada ya ukaguzi huo, Mhe. Senyamule amewataka wasimamizi wa maandalizi kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miundombinu yote muhimu, hususan lango kuu la kuingilia, ili viwanja hivyo viwe katika hali nzuri na viwe tayari kupokea washiriki na wageni watakaohudhuria maonesho hayo.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuboresha na kukamilisha huduma zote za kijamii, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, umeme wa uhakika, vyoo vya kutosha, usafi wa mazingira pamoja na huduma nyingine muhimu, ili kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi na wadau watakaoshiriki Maonesho hayo.
"Maandalizi mazuri yataongeza hadhi ya Maonesho ya Nanenane na kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Kilimo kuonesha teknolojia, ubunifu na mafanikio yanayochochea maendeleo ya uchumi na kuimarisha usalama wa chakula," amesema Mhe. Senyamule.
Ameongeza kuwa maandalizi ya mapema na ushirikiano wa wadau wote ni msingi wa kufanikisha Maonesho ya Nanenane, ambayo yanalenga kuonesha mafanikio, ubunifu na teknolojia mbalimbali katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, sambamba na kuwakutanisha wadau kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujenga fursa za maendeleo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ugani, Wizara ya Kilimo, Bi. Upendo Mndeme, amesema maandalizi yote yanatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 16, 2026. Ameeleza kuwa maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi kwa wakati ili kuhakikisha viwanja vinakuwa tayari kwa ajili ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) mwaka huu.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA KWA MAKINI MIRADI YA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amezielekeza Halmashauri zote Nchini, kutambua na kusimamia ipasavyo miradi ya miundombinu ya elimu kwa kidato cha tano na sita inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick kupitia Twiga Minerals Corporation, kwa kiwango sawa na miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali.
Akizungumza Julai 2, 2026, wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa, Prof. Shemdoe amesema Halmashauri zinapaswa kuhakikisha usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa miradi hiyo, ikiwemo kuratibu kazi za wazabuni na wakandarasi ili kuhakikisha ubora wa kazi na kasi ya utekelezaji.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu endelevu wa matengenezo ya majengo, vifaa na miundombinu ya shule ili kudumisha ubora wa huduma za elimu.
Kwa upande wake, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Bw. Atupele Mwambene, amesema mradi huo unalenga kuongeza nafasi za wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na sita kupitia ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Janeth Mayanja amesema mkoani Dodoma mradi huo umetekelezwa katika shule 4 za sekondari zilizopo Wilaya za Kongwa, Chemba na Bahi, hatua iliyobooresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kuongeza fursa za wanafunzi kupata elimu bora.
Naye Mwakilishi wa Meneja Mkazi wa Barrick Tanzania na Meneja wa Fedha wa kampuni hiyo, Bi. Penina Kituku, amesema uwekezaji huo unaonesha dhamira ya kuendelea kuwekeza katika elimu, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa.
Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Barrick kupitia mchango wa Dola za Marekani milioni 30, na hadi sasa umewezesha ujenzi wa madarasa 1,090, mabweni 270 na matundu ya vyoo 1,640 katika maeneo mbalimbali Nchini.Ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi katika kuimarisha sekta ya elimu na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
RC SENYAMULE AZINDUA LANDMAX REAL ESTATE, AITANGAZA DODOMA KUWA KITOVU CHA UWEKEZAJI
Na Mwandishi Wetu, DODOMA RS.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, leo Juni 24, 2026 amezindua rasmi kampuni ya Landmax Real Estate Company Limited, inayojihusisha na uuzaji wa nyumba, viwanja pamoja na upangishaji wa nyumba za makazi (apartments).
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Senyamule amesema hatua hiyo ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji na biashara katika Mkoa wa Dodoma.
"Dodoma inaendelea kukua kwa kasi kutokana na uwekezaji unaofanyika katika sekta mbalimbali za uchumi, huku Serikali ikiendelea kuboresha miundombinu na huduma za kijamii, jambo lililoifanya kuwa kitovu muhimu cha uwekezaji Nchini.
Sekta ya ardhi na nyumba ni miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi, hivyo uwepo wa Landmax Real Estate Company Limited utaongeza chachu ya maendeleo kwa kutoa huduma bora na za kitaalamu katika masuala ya ardhi na uwekezaji"- Amesema Mhe. Senyamule
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, uwazi na weledi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, huku akiwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza mkoani Dodoma kutokana na fursa nyingi za kiuchumi na mazingira mazuri ya biashara yaliyopo.
Alieleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule alimpongeza mwanzilishi wa Landmax Real Estate Company Limited kwa uamuzi wake wa kuwekeza Dodoma, akisema kampuni hiyo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazohusiana na umiliki wa ardhi, nyumba na uwekezaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, Mhe. Onesmo Mnkondya, amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora, salama, zenye uwazi na matokeo chanya.
Amesema mafanikio hujengwa kwa ushirikiano, hivyo amewaomba wadau wote wa sekta ya ardhi kuiunga mkono kampuni hiyo ili kuchangia maendeleo ya Jiji la Dodoma, kuboresha utoaji wa huduma na kujenga mahusiano bora na jamii.
DODOMA RS TV CHANNEL

#DodomaFahariYaWatanzania
#KeroYakoWajibuWanguTabasamuNaSamia
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#Nanenane2026
2 months ago | [YT] | 2
View 0 replies

2 months ago | [YT] | 0

#WekezaDodomaStawishaDodoma
#KeroYakoWajibuWanguTabasamunaSamia
#KazinaUtuTunasongaMbele.
2 months ago | [YT] | 0
View 0 replies
DODOMA RS TV CHANNEL
RC SENYAMULE AZINDUA LANDMAX REAL ESTATE, AITANGAZA DODOMA KUWA KITOVU CHA UWEKEZAJI
Na Mwandishi Wetu,
DODOMA RS.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, leo Juni 24, 2026 amezindua rasmi kampuni ya Landmax Real Estate Company Limited, inayojihusisha na uuzaji wa nyumba, viwanja pamoja na upangishaji wa nyumba za makazi (apartments).
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Senyamule amesema hatua hiyo ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji na biashara katika Mkoa wa Dodoma.
"Dodoma inaendelea kukua kwa kasi kutokana na uwekezaji unaofanyika katika sekta mbalimbali za uchumi, huku Serikali ikiendelea kuboresha miundombinu na huduma za kijamii, jambo lililoifanya kuwa kitovu muhimu cha uwekezaji Nchini.
Sekta ya ardhi na nyumba ni miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi, hivyo uwepo wa Landmax Real Estate Company Limited utaongeza chachu ya maendeleo kwa kutoa huduma bora na za kitaalamu katika masuala ya ardhi na uwekezaji"- Amesema Mhe. Senyamule
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, uwazi na weledi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, huku akiwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza mkoani Dodoma kutokana na fursa nyingi za kiuchumi na mazingira mazuri ya biashara yaliyopo.
Alieleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule alimpongeza mwanzilishi wa Landmax Real Estate Company Limited kwa uamuzi wake wa kuwekeza Dodoma, akisema kampuni hiyo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazohusiana na umiliki wa ardhi, nyumba na uwekezaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, Mhe. Onesmo Mnkondya, amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora, salama, zenye uwazi na matokeo chanya.
Amesema mafanikio hujengwa kwa ushirikiano, hivyo amewaomba wadau wote wa sekta ya ardhi kuiunga mkono kampuni hiyo ili kuchangia maendeleo ya Jiji la Dodoma, kuboresha utoaji wa huduma na kujenga mahusiano bora na jamii.
#DodomaFahariyaWatanzania
#WekezaDodomaStawishaDodoma
2 months ago | [YT] | 1
View 0 replies