Deutsche Welle ni Shirika la Kimataifa la Utangazaji la Ujerumani, linaloandaa vipindi vya Televisheni, Radio na Mtandao wa Intaneti kwa ajili yako katika lugha 30 - popote ulipo ulimwenguni.

Tafadhali tusaidie kuyafanya majadiliano katika kituo hiki kuwa safi na ya kukubalika na jiepushe kutumia lugha ya kibaguzi au uchafu pamoja na matusi ya kibinafsi.

Kwa taarifa zaidi tafadhali bonyeza link ya "DW Netiquette" hapo chini.

www.dw.com/en/dws-netiquette-policy/a-5300954


DW Kiswahili

Baada ya kula vinono na kutumia hela nyingi kwenye sherehe za Sikukuu, wengi hujikuta katika hali ya kutoweza kutimiza majukumu mengine yanayohitaji fedha ipasavyo. Je, wewe umejipanga vipi? Je mchoro wa Said Michael unaakisi hali halisi?

1 week ago | [YT] | 56

DW Kiswahili

Taswira ya vihunzi katika safari ya urais wa Samia muhula wa pili.

4 weeks ago | [YT] | 73

DW Kiswahili

Daktari mmoja nchini Tanzania amekiri kwamba mamia ya wagonjwa na maiti walichukuliwa kutoka hospitali na kupelekwa kwenye maeneo yasiyojulikana, matamshi yaliyochochea miito zaidi ya maandamano yanayotarajiwa Disemba 9.



Daktari huyo mwandamizi kutoka hospitali kubwa jijini Dar es Salaam, aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotambulishwa amesema waliagizwa kutosema chochote, na simu zao zilichukuliwa na kuchunguzwa kama zilikuwa na picha ama video yoyote.



Amesema wakati akiwa kwenye zamu Novemba Mosi, zaidi ya wagonjwa wake 200 walichukuliwa na watu ambao hawakuwa wamevalia sare yoyote, waliofika hospitalini na malori ya rangi ya kijani inayofanana na rangi ya jeshi.


Ameongeza kuwa walichukua miili iliyokuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, kilichokuwa kimefurika, hadi miili mingine kulazwa chini na kulingana na mfanyakazi mmoja wa chumba hicho, zaidi ya miili 300 ilichukuliwa.

1 month ago | [YT] | 225

DW Kiswahili

Tafakari ya kauli ya Msema wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa aliyoitoa jana kuhusu vyombo vya habari vya kimataifa kuchapisha habari ya upande mmoja.

1 month ago | [YT] | 336

DW Kiswahili

Baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuindua rasmi Tume ya Uchunguzi wa vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, mchora katuni wetu Said Michael ameibuka na mchoro huu. Je, tume hiyo italeta majibu ya kweli? Ipi tafsiri yako kuhusu katuni hii? #DWKatuni

1 month ago | [YT] | 221

DW Kiswahili

Je, unajua kuwa mamilioni ya watu duniani bado hawana choo salama?
Na je, unajua madhara ya kufungulia vyoo wakati wa mvua?
Je, unadhani ni kwa nini bado baadhi ya watu hufungulia vyoo msimu huu?
Vyoo visivyo salama vinaweza kusababisha magonjwa hatari kama kipindupindu, kuhatarisha maisha ya watoto, na kudhalilisha utu wa binadamu. Kila mtu anastahili choo salama, safi na chenye heshima.
Tupe maoni yako ⬇️ #SikuYaChooDuniani #UsafiWaMazinga #AfyaKwaWote

1 month ago | [YT] | 37

DW Kiswahili

Mtizamo wa mchambuzi wa siasa kuhusu hatua ya Rais Samia kumteua mwanaye na pia Paul Makonda katika baraza la mawaziri: www.youtube.com/shorts/Ul-kNF...

1 month ago | [YT] | 0

DW Kiswahili

Baba huyu wa Uganda anaonyesha upendo kwa mtoto wake njiti

1 month ago | [YT] | 0

DW Kiswahili

Mchambuzi wa siasa Gwandumi Mwakatobe amweka Mwigulu Nchemba kwenye darubini https://www.youtube.com/watch?v=S2_P4...

1 month ago | [YT] | 5

DW Kiswahili

Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania. Je unafahamu nini kumhusu? Tizama vidio hii kisha utuachie maoni yak au ujumbe wako kwake. www.youtube.com/shorts/BAkqzH...

1 month ago | [YT] | 25