utoto mtakatifu parokia ya mt yoseph-nansio

watoto wa Shirika la Kipapa Parokia ya Mtakatifu Yoseph Baba Mlishi nansio pia tupo
www.facebook.com/share/g/1JtUGx3m27/
youtube.com/@utotomtakatifuparokiayamtyosep?si=Pza…


utoto mtakatifu parokia ya mt yoseph-nansio

MASOMO YA MISA,
SIKU YA JUMAPILI
FEBRUARI 8, 2026
DOMINIKA YA 5 YA MWAKA A WA KANISA

MWANZO:
Zab. 95:6 – 7
Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba; kwa maana ndiye Mungu wetu.

SOMO 1
Isa. 58:7 – 10

Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 112:4 – 9 (K) 4

(K) Nuru huwazukia wenye adili gizani.

Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
Heri atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye mambo yake kwa haki. (K)

Kwa maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye haki atakumbukwa milele.
Hataogopa habari mbaya;
Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. (K)

Moyo wake umethibitika hataogopa,
Hata awaone watesi wake wameshindwa.
Amekirimu na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu. (K)

SOMO 2
1Kor. 2:1 – 5

Ndugu zangu, mimi nilipopkuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili Imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Mdo. 16:14

Aleluya, aleluya,
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
Aleluya.

INJILI
Mt. 5:13 – 16

Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu yam lima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

5 days ago | [YT] | 2

utoto mtakatifu parokia ya mt yoseph-nansio

KARIBU CHANNEL YETU #SUBSCRIBED UWEZEKUPATA MATUKIO MENGI UBARIKIWE
MASOMO YA MISA,
FEBRUARI 6, 2026
SIKU YA IJUMAA
JUMA LA 4 MWAKA A WA KANISA

KUMBUKUMBU YA WAT. PAULO MIKI NA WENZAKE (Shahidi)

SOMO 1
Ybs. 47:2-11

Kama mafuta yalivyotengwa na kafara ya amani, vivyo hivyo Daudi alitengwa na wana wa Israeli. Naye alicheza pamoja na samba kana kwamba ni wana-mbuzi, pia pamoja na dubu kana kwamba ni wana-kondoo wa kundi.
Je! Hakumwua jitu katika ujana wake, Akawaondolea watu lawama; Alipouinua mkono wake na jiwe la teo, Akayashusha majivuno ya Goliathi? Kwa maana alimwita Aliye juu; Na Yeye akaitia nguvu yamini yake; Ili amwue shujaa hodari wa vita; Ili aiinue pembe ya watu wake.Kwa hiyo binti za watu wakamtukuza wakiimbiana, na kumheshimu alivyoua makumi elfu yake; naye alipokwisha kuivaa taji ya utukufu, alipigana na adui na kuwashinda pande zote; akajenga maboma yake kati ya Wafilisti, akaivunja pembe yao vipande vipande, hata siku hii ya leo.Katika kila kazi yakeDaudi alimshukuru Mungu Aliye juu kwa maneno matukufu; na kwa moyo wake wote akampenda Mola wake, akamhimidi kila siku daima. Pia akaweka waimbaji mbele ya madhabahu, ili watoe sauti tamu katika kuimba kwao.Akauongeza uzuri wa sikukuu, akaziratibisha nyakati katika ukamilifu; pindi walipolihimidi jina takatifu la Bwana, hata patakatifu pakavuma sauti tokea asubuhi na mapema. Naye Bwana akamwondolea dhambi zake, akaiinua pembe yake hata milele; akampa agano la ufalme, na kiti kitakatifu cha enzi katika Israeli.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 18:30, 46, 49-50 (K) 46

(K) Atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.

Mungu njia yake ni kamilifu,
Ahadi ya Bwana imehakikishwa,
Yeye ndiye ngao yao wote wanaomkimbilia. (K)

Bwana ndiye aliye hai, na ahimidiwe mwamba wangu,
Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.
Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa.
Nami nitaliimbia jina lako. (K)

Ampa mfalme wake wokovu mkuu,
Amfanyia fadhili masihi wake,
Daudi na mzao wake hata milele. (K)

SHANGILIO
Lk. 8:15

Aleluya, aleluya,
Heri wale ambao kwa unyofu na wema wa moyo hulishika neno la Mungu, kasha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Aleluya.

INJILI
Mk. 6:14-29

Mfalme Herode alisikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa kutangaa, akasema, Yohane Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii. Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohane mwenyewe alikuwa amefufuka.Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohane, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake; kwa kuwa amemwoa; kwa sababu Yohane alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Maana Herode alimwogopa Yohane; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji.Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi, akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye.Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

6 days ago | [YT] | 1